Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Afrika amesema umoja huo unakabiliwa na changamoto ya matatizo ya
kifedha na taathira zake mbaya katika utekelezaji wa operesheni za
kulinda amani.
Erastus Mwencha ameeleza wasiwasi kuhusu hali ya kifedha ya
Umoja wa Afrika na kusema, kwa sasa umoja huo unasumbuliwa na changamoto
kubwa za kudhamini gharama na bajeti ya operesheni zake katika nchi za
Afrika hususan bajeti ya kikosi cha kulinda amani nchini Somalia
(AMISOM).
Mwencha ameongeza kuwa, hali hiyo imetokana na kutotengwa bajeti kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini SomaliaNaibu Mweyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesema, tangu miaka 9
iliyopita Umoja wa Afrika ulituma askari wake nchini Somalia kwa ajili
ya kupambana na na ugaidi na kwamba uhaba wa fedha, zana na vitendea
kazi wa taasisi hiyo unatia wasiwasi.
Zaidi ya wanajeshi elfu 22 wa Umoja wa Afrika wamepelekwa Somalia kwa
ajili ya kupambana na kundi la kigaidi la al Shabab na kurejesha amani
katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni