Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema
jumuiya hiyo ya kimataifa ina wasiwasi mkubwa kuhusu ubaguzi unaowalenga
wahajiri na jamii za waliowachache.
António Guterres amesema, kwa sasa mitazamo ya taasubi inaenea
kwa kasi na kufungua njia ya chuki na uadui, hivyo jamii ya kimataifa
inalazimika kuwa makini na macho.
Guterres amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kuimarisha taasisi zake
katika masuala ya haki za binadamu na vilevile kutekeleza uadilifu dhidi
ya wale wanaofanya jinai kubwa dhidi ya binadamu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mitazamo ya kibaguzi ambayo hii leo inawalenga Waislamu inahuzunisha sana. Maandamano dhidi ya siasa za kibaguzi za Donald Trump
Matamshi hayo ya António Guterres yametolewa wakati Rais mpya wa
Marekani, Donald Trump amezidisha siasa zake za kibaguzi na kiadui dhidi
ya wahajiri na Waislamu.
Ijumaa ya jana Trump alitia saini amri ya kuwazuia Waislamu kuingia
nchini humo. Wakati wa kampeni zake za uchaguzi, Trump alitoa wito wa
kuzuiwa kikamilifu Waisalmu kuingia Marekani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni