Hussein Naqavi Husseini ambaye alikuwa akizungumzia hatua ya
Rais wa Marekani na kusaini sheria ya kuzuia visa ya kuingia nchini
Marekani raia wa nchi 7 za Kiislamu ikiwemo Iran, amesema hatua hiyo ni
kinyume na madai ya serikali ya Washington eti inaheshimu demokrasia,
uhuru wa kupata habari, haki za binadamu na mahusiano baina ya watu wa
nchi mbalimbali.
Naqavi Husseini ameongea kuwa, hatua ya Trump ya kupiga marufuku viza
kwa raia wa nchi kadhaa za Kiislamu ni kielelezo cha wazi zaidi cha
ubaguzi wa kizazi na kidini.
Msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Bunge la
Iran amesema kuwa, hatua hiyo ya Trump ya kuwalenga Waislamu ni uungaji
mkono wa sera za kuhujumu na kupiga vita Uislamu na Waislamu nchini
Marekani.
Siku chache zilizopita mfuasi wa Rais Trump kutoka Massachusetts alimshambulia na kumjeruhi mwanamke Mwislamu katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa John F. Kennedy mjini New York.
Robin Rhodes alimshambulia kwa maneno makali na kumpiga teke mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina Rabeeya Khan, mfanyakazi wa shirika la ndege la Delta Airline kutokana na chuki za kidini na kikaumu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni