Kamishna wa Kanda Maalum ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro amesema matukio ya Ubakaji na Ulawiti yameongezeka kwa kiwango kikubwa katika mwaka wa 2016 ukilinganisha na mwaka 2015 kutokana na matukio yaliyolipotiwa kiwa kipindi cha mwaka mzima.
Amesema
hii inatokana na kuanzishwa kwa Dawati la Jinsia na pia wananchi kupata
uelewa na kuripoti matukio hayo kila yanapotokea hii ndiyo sababu kubwa
inayofanya kuongezeka kwa matukio hayo katika mkoa wa Dar es salaam.
Kamishna
Saimon Sirro akizungumza katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati jijini Dar
es salaam ametoa taarifa hiyo wakati akielezea takwimu za matukio
mbalimbali yaliyotokea kwa mwaka 2016.
Kamishna
wa Kanda Maalum ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro
amesema mwaka 2015 vitendo vya ubakaji vilivyoripotiwa vilikuwa 972
wakati mwaka 2016 vitendo vya kubaka vilivyoripotiwa vilikuwa 1030
ambapo ongezeko lilikuwa ni asilimia 58 ukilinganisha na matukio hayo
kwa mwaka 2015.
Akitoa
takwimu za vitendo vya kulawiti kwa mwaka 2015 amesema vitendo vya
ulawiti vilivyoripotiwa ni 3010 ambapo mwaka 2016 vitendo hivyo
viliripotiwa kwa matukio 383 sawa na asilimia 73.
Amewataka wananchi kuacha matendo maovu kwani hayatawafikisha popote zaidi ya kuishia katika mikono ya sheria na kutupwa jela.
Kamishna
wa Kanda Maalum ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro
aksisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika
kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam.
Diana
Masala Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania TRA akizungumzia msako uliofanywa kati ya Mamlaka hiyo
na Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama ambapo ulifanikisha
kukamata bidhaa mbalimbali za magendo.
Kamishna
wa Kanda Maalum ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro
akiangalia silaha mbalimbali zilizokamatwa katika misako mbalimbali ya
pilisi mwaka 2016.
Kamishna
wa Kanda Maalum ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro
akieleza jambo kwa wanahabari wakati alipokuwa akionyesha silaha hizo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni