TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumatatu, 3 Oktoba 2016

TUMIENI FURSA KURASIMISHA BIASHARA

Hakuna maoni
OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Frank Kanyusi, amewataka wafanyabiashara kuendelea kujitokeza kwa wingi na kutumia nafasi hiyo adimu kurasimisha shughuli zao.
Alisema Wakala huo, umepata mafanikio makubwa katika ziara za kuhamasisha wafanyabiashara mikoani Mwanza, Mara na Geita na ziara hiyo inaendelea katika mkoa wa Simiyu, Shinyanga na Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Kanyusi alisema, taasisi yake imejipanga kuendelea kutoa elimu stahiki na kuhamasisha wafanyabiashara kujitokeza na kurasimisha shughuli zao.
Aliwataka wajasiriamali, wafanyabiashara na Watanzania wote wa mikoa hiyo, wafike kupata elimu ya namna ya kurasimisha biashara zao na kuzifahamu huduma nyingine zinazotolewa na wakala kwa njia ya mtandao.
Alisema Oktoba 3 hadi 8, mwaka huu, watakuwa mkoa wa Simiyu, Oktoba 10 hadi 15, mkoa wa Shinyanga na Oktoba 17 hadi 22, watakuwa mkoa wa Tabora.
Alifafanua kwamba kuna faida nyingi za kurasimisha biashara, ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na serikali, kupata fursa mbalimbali, kuwa na walipa kodi wengi na kodi zao kutumika katika ujenzi wa taifa na huduma za jamii.
Katika mkoa wa Mwanza, kampuni 100 na majina ya biashara 150 yalisajiliwa, Geita majina ya biashara 60 na kampuni 50 na Mara majina ya biashara 45 na kampuni 30

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni