TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumatatu, 3 Oktoba 2016

RAISI KABILA AZURU NCHINI TANZANIA

Hakuna maoni
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila amewasili Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
Amepokelewa na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo rais John Magufuli, makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania balozi Augustine Mahiga , Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi mbalimbali wa Serikali, Mabalozi na wananchi.
Rais Joseph Kabila akiwasili katika katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere nchini Tanzaniamage caption
Rais Joseph Kabila akiwasili katika katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere nchini Tanzania
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Joseph Kabila Kabange amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na baadaye kushuhudia burudani ya vikundi vya ngoma.
Siku ya Jumanne tarehe 04 Oktoba, 2016 rais Joseph Kabila Kabange atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, ataweka jiwe la msingi la jengo la mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadaye kushiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika ziara yake Rais Kabila anatarajia pia kuzungumzia masuala ya kisiasa nchini mwake ambapo uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu umesogezwa mbele mpaka mwakani jambo ambalo limeleta sintofahamu kwa wananchi wa Kongo.
Kabila ataondoka siku ya Jumatano kurudi Kinshasa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni