Makamu wa rais nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa kuweka huduma ya mtandao wa Wi-Fi katika maeneo ya umma na yale ya burudani mjini Dar es Salaam.
Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini humo utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyobasi kuimarisha uchumi.
''Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani,watu wataweza kupata huduma ya mtandao'' ,alisema.
Kwa upande wake Kamishna wa Jimbo la Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa mradi huo ni mmoja wa awamu tano za juhudi za serikali kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.
Utekelezaji wa mradi huo ndio mwanzo wa safari ya kujenga miji na miji mikuu katika kiwango cha 'Smart City'.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni