TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumanne, 4 Oktoba 2016

KOCHA WA NDANDA ROHO KWATU

Hakuna maoni
KOCHA mkuu wa timu ya Ndanda ya Mtwara, Mohamed Abdallah ameipongeza timu yake kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Toto Africa katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani hapa.
Kocha Abdallah alisema vijana wake walicheza vizuri kwa kufuata maelezo yake na ndio maana wakaibuka na ushindi.
“Nashukuru sana kwa vijana wangu tumepata pointi tatu, tuliharibu mechi yetu dhidi ya Mbao ila baada ya kuona matatizo yetu katika mchezo uliopita nimeenda kurekebisha makosa yetu na mafanikio yameonekana,” alisema.
Aidha, kocha huyo alimlaumu mwamuzi Jonesia Rukya kutoka Kagera kwa kumpa kadi ya njano nahodha wa timu yake Kiggi Makasi.
Mchezo unaofuata Ndanda inatarajia kucheza na African Lyon jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa timu hiyo ya Mtwara ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni