Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi DK.Charles Tibeza |
Alitoa agizo hilo jana alipokuwa akifungua Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini hapa na kuhudhuriwa na wadau kutoka halmashauri za mikoa saba ya kanda hiyo.
Alisema miongoni mwa wateja wasionufaika na kile wanachonunua kutokana na kutojua ni kwa kiasi gani wamehudumiwa, ni walaji wa nyama hususani zinazochomwa kwa kuwa wauzaji hutumia njia ya kukadiria badala ya kuwapimia.
Alisema jambo la kushangaza ni kuwa wauzaji hao wa nyama choma huchukua bidhaa hizo kwenye bucha na machinjio zikiwa zimepimwa, lakini wao hawataki kuwatendea haki wateja wao kwa kuwapimia kwa kipimo kinachotakiwa, hivyo ni sawa na kuwaibia wateja.
Amewataka WMA kusimamia mfumo wa matumizi wa vipimo vinavyotakiwa katika maeneo yote ikiwemo kwenye masoko ya bidhaa kama kuku, nyanya na vitunguu akisema bado mfanyabiashara ananeemeka kwa kuwanyonya wakulima na wateja wake.
Alisema serikali haiko tayari kuona vipimo vya makopo na ndoo vikiendelea kutumika bali kila Mtanzania anapaswa awajibike kwa kuhakikisha kwenye eneo lake matumizi ya vipimo sahihi yanazingatiwa ili kuleta usawa katika uchumi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni