Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe John Pombe Magufuli amesema serikali yake imepunguza makato
ya kodi katika mishahara kutoka asilimia 11 mpaka 9 ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa kada hiyo huku akiahidi fedha
zinazokusanywa katika vita ya ufisadi, ukwepaji kodi na watumishi hewa
zitapelekwa kwenye miradi ya maendeleo na kuboresha maslahi
ya wafanyakazi ili kuongeza tija na ufanisi makazini.
ya wafanyakazi ili kuongeza tija na ufanisi makazini.
Rais John Magufuli anatoa kauli hiyo katika maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi duniani ambayo kitaifa yamefanyika mjini dodoma ikiwa ni
mara yake ya kwanza tangu kuapishwa kuwa Rais ambapo anasema hatua hiyo
itsaidia kupunguza ukali wa maisha hasa kwa wafanyakazi wa kawaida huku
pia akitoa wito wa kufanya kazi kwa bidii.
Huku akishangiliwa na umati wa watu katika risala yake Rais
Magufuli akatoa takwimu mpya za vita dhidi ya wafanyakazi hewa ambapo
amesema hivi sasa wamefikia zaidi ya elfu kumi na bado mapambano
yanaendelea.
Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA
Nicholaus Mgaya amesema bado sekta ya ajira nchini inakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo ongezeko la wageni kupora kazi za wazawa huku
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, vijana ajira na
walemavu, Mh.Jenista Mhagama akibainisha kuwa serikali iko katika
mkakati wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na viwango
vilivyowekwa na shirika la kazi duniani (ILO).
Nao baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wamepongeza kasi ya
utendaji wa serikali ya awamu ya tano wakidai kuwa itakuwa chachu ya
maendeleo kwa taifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni