Mwanasheria wa rais wa Marekani, Donald Trump amemjia juu msanii wa
muziki wa hip hop, Snoop Dogg baada ya kuachia video yake mpya ya
‘Lavender’ akiwa anamwonyeshea bastola Donald Trump wa uwongo ambae ametumika ndani ya video hiyo.
Michael Cohen ambaye ni mwanasheria wa Donald Trump kupitia
mazungumzoyake aliyoyafanya na mtandao wa TMZ, alifunguka kwa kusema
kwamba kitendo ambacho amekifanya Snoop Dogg ni udhalilishaji kwa Rais
Donald Trump na kusema kwamba Snoop anapaswa kuomba msamaha kwa kitendo
chake hicho.
Ni sawa kufanya utani lakini kwa upande wa Snoop Dogg amevuka mipaka
ya utani kwa kile kikubwa ambacho alikifanya cha kutoa pisto ya uongo na
kuinyoosha kwa mfano huo wa Donald Trump huku ikiwa imeandikwa ‘Banng’,
Cohen anasema kwamba hakuna utani wa mauaji kwa Rais na kitendo hiko
kimemshtua sana mwanasheria huyo wa Trump.
“Nisingeweza kulikubali jambo hilo hata kama Raisi angekuwa ni Barack
Obama, na vilevile siwezi kukubali hata kwa Donald Trump, unajua kitu
ambacho kinanisikitisha kwa Snoop Dogg ni kwamba kuna vitu vingi sana
ambavyo angeweza kuvifanya kwa jamii lakini sio kwa video hii” aliongea
Michael Cohen.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni