Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limewataka wasanii wa muziki nchini
kufuata taratibu za kupeleka nyimbo zao kukaguliwa kabla hazijatoka ili
kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara kwa baadhi ya
wasanii ambao wamekuwa wakitoa nyimbo bila kukaguliwa na baadaye
kufungiwa na baraza hilo kutokana na kukosa maadili.
Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Basata, Agnes Kimwaga alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika semima maalum ya mazunzo juu
kutambua shughuli mbalimbali zinazofanya na baraza hiyo.
Alisema wasanii wote wanatakiwa kuwasilisha kazi zao Basata ili
zikaguliwe kabla ya kutoka na pia kushauriana namna nzuri ya kuufikisha
ujumbe wao kwa jamii bila kuvunja utaratibu.
“Mpaka sasa wasanii ambao wanaleta kazi zao kukagulia ni Nay wa
Mitego tena baada ya kupata misukosuko lakini kwa sasa kabla ya kutoa
kazi analeta ikagulie, pia na Professor analetaga,” alisema Kimwaga.
Aidha alisema baraza hilo lipo kwajili ya wasanii hivyo wasanii wanatakiwa kulitumia ili kustawisha sanaa ya muziki nchini.
Pia alisema Baraza hili linatoa msaada wa kisheria pamoja na wakibishara kwa wasanii ambao watahitaji.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni