Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dr Shein, amesema hatishwi na vitisho vya
TANESCO vya kuikatia umeme Zanzibar kwa sababu ya deni la Umeme kwani
deni sio la leo, deni lina zaidi ya miaka 20.
Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa
habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka
Indonesia ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na
bahari ya Hindi akiwakilisha Rais John Magufuli ambapo amesema deni
linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yeyote ya
Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.
“Tungoje basi uzimwe kama nyie muna wasiwasi, mimi najua hawezi
kuuzima, kwa sababu deni hatujaanza kudaiwa leo sisi. Miaka 20 imepita
tunadaiwa, kwahiyo mimi sitaki niseme sana leo kwenye hili na kama
watazima basi, tutawasha vibatari vyetu, hatuna tatizo sisi. Lakini
sidhani Tanzania iliyomakini kama inaweza kufanya vitu kama hivyo na
sina uhakika kama magazeti yameandika vizuri,” alisema Dkt. Shein
Hatua hiyo imekuja baada ya TANESCO kutoa siku 14 kwa wadaiwa Sugu wa
umeme kulipa vinginevyo watakaitwa umeme. Zanzibar inadaiwa deni la
umeme zaidi ya Bil 121.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni