Mh Temba amefunguka sababu ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki.
Msanii huyo amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa alitakiwa
kuachia wimbo mpya mapema kabala hata ya ‘Acha Waoane’ wa Chege lakini
kuna vitu viliingiliana vikavuruga ratiba hiyo.
Temba amevitaja vitu hivyo ni pamoja na kuibiwa fedha zake na zingine
za baadhi ya marafiki zake ambazo alitegemea kufanyia kazi kwenye
muziki ikiwemo kutumika kwenye kutengenezea video.
Rapper huyo amemtaja aliyewaibia anaitwa Mustafa Andumbotela
Ndingubita na ameahidi kutoa kiasi cha milioni moja kwa mtu
atakayesaidia kukamatwa kwake huku naye Chege akiongezea kiasi cha laki
tano kwenye zawadi hiyo ambapo itakuwa ni milioni moja na nusu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni