TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumatatu, 5 Desemba 2016

WAGONJWA WENYE MATATIZO YA AKILI WAKIMBIA HOSPITALI KENYA

Hakuna maoni
Huduma katika hospitali za serikali zimeathiriwa na mgomo
Image captionHuduma katika hospitali za serikali zimeathiriwa na mgomo
Wagonjwa kadha wenye matatizo ya kiakili wameitoroka hospitali kuu ya wagonjwa wenye matatizo ya kiakili nchini Kenya, hospitali ya Mathari jijini Nairobi.
Taarifa za vyombo vya habari zinasema huenda wagonjwa hao wametumia fursa ya kutokuwepo kwa madaktari wanaogoma kutoroka.
Polisi wanawasaka wagonjwa hao.
Gazeti la Nation linasema wagonjwa waliotoroka ni karibu 50 ingawa Standard linaripoti kwamba huenda wakafikia 100.
Madaktari na wauguzi kote nchini Kenya wanagoma kuishinikiza serikali iwalipe malimbikizi ya nyongeza ya mishahara na marupurupu mengine chini ya makubaliano yaliyotiwa saini Juni mwaka 2013.
Mgomo huo umeathiri hospitali zote zinazoendeshwa na serikali za majimbo pamoja na hospitali kuu za rufaa - Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Hospitali ya Moi mjini Eldoret.
Daktari aliyebebea bango
Maafisa wakuu wa afya serikali walifanya mkutano wa dharura Jumapili usiku kujaribu kuzuia mgomo huo lakini juhudi zao hazikufua dafu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni