TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumatano, 9 Novemba 2016

MOURINHO HAPENDEWZI NA IDARA YA MATIBABU UNITED

Hakuna maoni
Mkufunzi wa man United Jose Mourinho
Image captionMkufunzi wa man United Jose Mourinho
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anachunguza kila kitu kuhusu kikosi chake cha kwanza baada ya kusikitishwa na utamaduni aliorithi katika klabu hiyo.
Mourinho inadaiwa haifurahii idara ya matibabu ya klabu hiyo.
Lakini baada ya kumrithi Louis Van Gaal msimu uliopita,inaeleweka kwamba Mourinho anahisi utamaduni uliopo katika klabu hiyo hauafikii matarajio yake.
Mourinho ameshinda mataji 23 akifunza Porto,Chelsea,Inter Milan na Real Madrid.
Raia huyo wa Ureno alishangazwa na hatua ya beki Luke Shaw mwenye umri wa miaka 21 na Chris Smalling mwenye umri wa mika 26 kwa kutoshiriki mechi dhidi ya Swansea ambayo United waliibuka washindi wa 3-2,akiambia vyombo vya habari kwamba lazima afanye chochote.
BBC Sport inaenlewa kwamba Mourinho mwenye umri wa miaka 53 anataka kudhibti kila eneo la timu hiyo ikiwemo usafiri mechi za kuajianda kwa msimu,maandalizi pamoja na kila kitu kinachojenga timu hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni