TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumatano, 9 Novemba 2016

CAF YAONGEZA FEDHA ZA WASHINDI KATIKA MASHINDANO YAKE

Hakuna maoni
Shirikisho la soka barani Afrika Caf laongeza zawadi za fedha katika mashindano yakeImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionShirikisho la soka barani Afrika Caf laongeza zawadi za fedha katika mashindano yake
Shirikisho la soka barani Afrika Caf limeongeza kitita cha fedha zinazozawadiwa washindi katika michuano yote kuanzia mwaka 2017 kueleka 2020.
Washindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika watapata dola milioni 4,wakati ambapo Ivory Coast ilizawadiwa dola milioni 1.5 iliposhinda taji hilo mwaka 2015.
Mshindi wa kombe la vilabu bingwa Afrika atajishindia dola milioni 2.5 badala ya dola milioni 1.5 ambazo Mamelodi Sundowns walijishindia mwezi uliopita.
Orodha ya fedha ambazo zitazawadiwa washindiImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionOrodha ya fedha ambazo zitazawadiwa washindi
Wakati huohuo fedha za mshindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika upande wa wanawake zitaongezwa na kufikia 80,000 mwaka 2019 kutoka dola 50,000 mwaka huu.
Fedha hizo ni chache mno ikilinganishwa na zile inazopewa timu iliomaliza ya mwisho katika kombe la bara Afrika upande wa wanaume.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni