![]() |
MKUU WA MKOA WA RUKWA ZELOTHE STEVEN |
WAFUNGWA na mahabusu katika gereza la mjini Sumbawanga, wameziomba mahakama nchini kumaliza kesi ndogo kwa kutoa adhabu za viboko badala ya kifungo ili kupunguza mrundikano wa mahabusu na wafungwa gerezani.
Walitoa ombi hilo huku baadhi wakitokwa na machozi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven, aliyetembelea gereza hilo juzi.
Zelothe aliyefika gerezani hapo kujionea kero na utendaji kazi, alitoa fursa kwa wafungwa 10 kuzungumzia kero zao baada ya wafungwa, Oswald Usambo, kusoma risala kwa niaba ya wenzake wakati wa ziara hiyo.
Wafungwa waliopewa nafasi baada ya risala hiyo walishauri kupunguza msongamano magerezani kwa mahakama kutoa adhabu za papo kwa hapo kama vile walevi kuchapwa viboko.
Baada ya kuwasikiliza wafungwa hao, Zelothe alimwamuru Mkuu wa Gereza hilo kuwa kila mfungwa apewe karatasi aandike yale aliyoyaona hakufanyiwa haki katika kesi zao zinazoendelea.
“Hamkuniita, nimeamua kuja mwenyewe kwa kuwa natambua wajibu wangu na pia nafuata maagizo ya Rais John Magufuli, na nimekuja na timu yangu ambayo sina wasiwasi nayo, hivyo kuweni watulivu na wavumilivu,” alisisitiza Zelothe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni