MKURUGENZI Mtendaji wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia amemuondoa katika nafasi yake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Levolosi, Dk Alexander Mchome na Mkuu wa Kitengo cha Meno, Dk Regina Masika kwa kushindwa kutoa huduma bora na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.
Amewaondoa watumishi hao kwenye nafasi hizo juzi baada ya ukaguzi wa kushtukiza, uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro na Mkurugenzi wa Jiji kituoni hapo Oktoba 8, mwaka huu na kubaini wagonjwa kukaa muda mrefu bila kupata huduma yoyote huku baadhi ya wataalamu wakifika kazini kwa muda wanaotaka.
Kutokana na kuondolewa katika nafasi hizo, alimtaka Dk Mchome kukabidhi ofisi kwa Dk Edward Feksi, ambaye kwa sasa atakuwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo; na pia alimtaka Dk Masika kukabidhi ofisi kwa Dk Eunice Minja, ambaye atakuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo hicho katika kituo hicho cha Levolosi.
Mkurugenzi huyo alitoa rai kwa watumishi wote wa idara ya afya, kufanya kazi kwa uaminifu, uadilifu na weledi katika kuwahudumia wananchi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni