TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Alhamisi, 11 Agosti 2016

WAFARIKI KATIKA MATUKIO TOFAUTI

Hakuna maoni
Kaimu kamanda mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira
Morogoro, ambapo wawili wamegongwa na basi la abiria kwenye barabara kuu ya Iringa- Morogoro na mwingine kuuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.

Aliyepigwa risasi ametambuliwa kuwa ni Godwin Salvatory ambaye Polisi inasema kuwa aliuliwa kwa bastola na majambazi waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki na kisha kupora Sh milioni 3.5 za mfanyabiashara wa Kihonda Bima, katika manispaa hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoani hapa, Leonce Rwegasira, alisema matukio hayo yalitokea Agosti 8, mwaka huu kwa nyakati tofauti, ambapo tukio la kwanza la uporaji wa kutumia silaha lilitokea saa 3:15 usiku katika eneo la Kihonda Bima.

Kamanda Rwegasira alisema kuwa watu wawili wanaume wasiofahamika wakitumia usafiri wa pikipiki aina ya Boxer wakiwa na silaha aina ya bastola walimvamia Teddy Nestory (32), mfanyabiashara na mkazi wa Kihonda Bima akiwa anarudi nyumbani kwake.

Alisema majambazi hao walifyatua risasi iliyomjeruhi Salvatory na kisha kupora fedha Sh milioni 3.5 na simu saba za aina tofauti zilizokuwa katika mkoba na kutokomea kusikojulikana.

 Kaimu Kamanda alisema majeruhi huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini alifariki dunia siku moja baadaye.
Alisema Polisi inaendelea kuwasaka majambazi hao.

Katika tukio la pili lililotokea Agosti 8, mwaka huu saa 2:00 usiku kwenye eneo la Kasanga Darajani, kwenye barabara kuu ya Iringa – Morogoro, Manispaa ya Morogoro kulitokea ajali iliyohusisha basi la abiria lenye namba za usajili T 988 CDC aina la Eicher mali ya Kampuni ya Islam, lilikokuwa likiendeshwa na Twaha Mponzi (35) mkazi wa Kihonda, Manispaa ya Morogoro, likitokea Ifakara kuelekea Morogoro.

Alisema basi hilo liligonga pikipiki yenye namba za usajili MC 164 BGE iliyokuwa ikiendeshwa na Jumanne Mussa (44) mkulima na mkazi wa Madaganya ikitokea Kasanga kuingia barabara kuu ya Iringa- Morogoro akiwa amempakia Levanus Leo (37) mkulima na mkazi wa Mindu.

Hivyo alisema ajali hiyo ilisababisha vifo vya papo hapo kwa wapanda pikipiki hao na miili yao imehifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Kaimu Kamanda huyo wa Polisi alisema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa pikipiki kuingia barabara kuu bila kuchukua tahadhari

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni