Madaktari wakiwa katika upasuaji wa mtoto wa jicho MOI |
Kambi hii iliyoanza Agosti 8, mwaka huu katika jengo la Wodi ya Watoto hospitalini hapo inatarajiwa kumalizika leo, lengo likiwa ni kuwafanyia upasuaji wagonjwa zaidi ya 60.
Mpaka jana tayari wagonjwa 30 walikuwa wameshafanyiwa upasuaji bure na madaktari hao ambao wanazunguka katika nchi tisa za Afrika kuendesha zoezi hilo la upasuaji wa mtoto wa jicho.
Nchi ambazo tayari wameendesha zoezi hilo ni Afrika Kusini, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia na Malawi.
Nchi nyingine ambazo wanatarajia kuendesha zoezi hilo baada ya kumaliza hapa nchini ni Kenya na Uganda.
Ofisa Mawasiliano wa Vision Care, Sun-hee Pak aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa ujumbe wa madaktari hao uliowasili nchini wiki iliyopita umejitolea kupunguza tatizo la mtoto wa jicho kwa nchi mbalimbali za Afrika ambazo zina uhusiano mzuri na Korea na wameahidi kurejea tena nchini mwakani.
Nao madaktari wa upasuaji wa macho katika Hospitali ya Muhimbili walisema programu hiyo itasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa ambao awali mgonjwa mmoja alitakiwa kulipa Sh 600,000 kwa ajili ya upasuaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni