Sasha
Obama, binti wa Rais wa Marekani Barack Obama ameingia kwenye headline
baada ya baadhi ya picha zake kusambaa mitandaoni zikimuonesha akiwa
kwenye mgahawa mmoja amevalia sare ya hoteli akifanya kazi. Vyombo vya
habari nchini Marekani vimeeleza kwamba ameamua kuacha ‘starehe’ za
ikulu ya White House na kuanza kufanya kazi katika mgahawa huo.
Binti huyo
mwenye umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja
katika mgahawa mmoja ulioko Martha’s Vineyard, Massachusetts. Gazeti la
Boston Herald limeripoti kuwa Sasha
ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliambatana na maafisa sita
wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni