Basi la kipekee lenye urefu wa mita mbili juu linaloruhusu magari ya
kibinafsi kupitia mvunguni mwake limefanyiwa majaribio katika mji wa
Hebei kaskazini mwa Uchina. Dhumuni kubwa la kutengeneza basi la aina
hiyo ni kutatua kabisa tatizo la usafiri kwa watu katika miji yenye
idadi kubwa ya wakazi.
Basi hilo linaloendeshwa kwa umeme linauwezo wa kubeba zaidi ya watu
300, lina urefu wa mita 21 na upana wa futi 25 na linauwezo wa kukimbia
kwa kasi ya Kilomita 60 kwa kila saa. Hii ni mara ya kwanza kwa wabunifu
kuonesha basi hilo hadharani baada ya video yake kuvuja katika mitandao
mwezi Mei.
Muonekano wa ndani ya basi hilo ambalo linanafasi kubwa mno ya kuweza hata kubeba abiria 300.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni