Maafisa wa
upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa
na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.
Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.
Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.
Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.
Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni