TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumapili, 5 Juni 2016

TANZANIA YAUNGA MKONO DUNIA KUDHIBITI TABAIANCHI

Hakuna maoni

TANZANIA kama zilivyo nchi nyingi zinazoendelea Afrika, imeunga mkono kupatikana kwa mkataba mpya unaolenga kudhibiti mabadiliko ya tabianchi duniani.
Bunge lilielezwa hayo hivi karibuni mjini hapa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga, wakati akiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo, kwa mwaka 2016/2017.
Makadirio ya bajeti hiyo ambayo Bunge liliyapitisha ni Sh 151,396,775,000. Balozi Mahiga

TANZANIA kama zilivyo nchi nyingi zinazoendelea Afrika, imeunga mkono kupatikana kwa mkataba mpya unaolenga kudhibiti mabadiliko ya tabianchi duniani.

Bunge lilielezwa hayo hivi karibuni mjini hapa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga, wakati akiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo, kwa mwaka 2016/2017.

Makadirio ya bajeti hiyo ambayo Bunge liliyapitisha ni Sh 151,396,775,000. Balozi Mahiga alisema, mkataba huo wa Paris, Ufaransa ulisainiwa mwishoni mwa mwaka jana.

Alisema tofauti na mikataba mingine iliyowahi kusainiwa katika vipindi vya nyuma, mkataba wa Paris umekuwa na nguvu zaidi kwa sababu una mamlaka ya kisheria kuzibana nchi zilizoendelea na zenye viwanda vingi kupunguza gesijoto.

“Mkataba huo uliokubaliwa na nchi zote, ulitiwa saini Aprili 22 mwaka huu kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York,” alisema.
Kwa mujibu wa Balozi Mahiga, nchi 175 zikiwemo zile kubwa ambazo zilikuwa zikipinga mikataba iliyopita nazo ziliukubali na kutia saini. Alisema Tanzania ilikuwa miongoni nchi zilizotia saini mkataba huo.

“Naomba nichukue fursa hii kuzisihi nchi zote hasa zilizoendelea na zinazotoa gesijoto kwa wingi kuheshimu makubaliano hayo ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kuitunza dunia yetu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema.
Katika hatua nyingine, amewataka Watanzania kulinda misitu, uoto wa asili na wanyamapori kwa sababu vyote hivyo vina manufaa kwa taifa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni