TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumapili, 8 Mei 2016

WILAYA YA KARAGWE WAPEWA TAHADHARI

Hakuna maoni



KAGERA
MK U U w a M k o a w a Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salim Kijuu ametoa siki 14 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kuhakikisha kazi ya utathmini wa majengo imefanyika na kisha apewe taarifa.
Alisema agizo hilo litazihusu halmashauri zote za mkoa huo kwani hilo ni agizo la serikali.Kijuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi, wananchi, wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo viongozi wa dini katika wilaya ya Karagwe ambapo alifanya ziara ya siku moja kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza changamoto zinazowakabili ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
“Serikali ilitoa muongozo wa kufanya tathmini ya haraka ya majengo ili kuziwezesha halmashauri kukusanya kodi za majengo (Property Tax) agizo hilo lilipaswa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu ambapo hadi sasa ukiachana na Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo hakuna halmashauri iliyowasilisha taarifa ya hatua waliyofikia katika utekelezaji wa agizo hilo, kwa hiyo natoa siku 14 agizo hilo liwe limetekelezeka na kunipa taarifa,”aliagiza Kijuu.
Alisema kuwa zipo changamoto za uhaba wa wataalamu katika Halmashauri lakini katika mamlaka ya Serikali za Mitaa wapo wataalamu wanaoweza kushirikishwa kwa halmashauri zisizo na wataalamu wakasaidia kufanikisha zoezi hilo, kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Kijuu alisema ni lazima watumishi na watendaji wa halmashauri na mkoa huo kujituma na kutoacha upenyo katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni