TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumamosi, 26 Machi 2016

WANAFUNZI WANNE WAMEFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI WILYNI KIBONDO MKOANI KIGOMA

Hakuna maoni
Wanafunzi wanne waliokufa baada ya kupigwa na radi katika kijiji cha Nyaruyoba Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, wamezikwa huku wananchi wakishauri serikali iziwekee kinga ya radi shule zake kutokana na mkoa wa kigoma kuwa na matukio kama haya kila mwaka.

 Wakizungumza katika mazishi hayo ,wamesema kutokana na kuwepo kwa matukio ya radi kila mwaka, ni vyema Serikali ikasaidia kuweka kinga ili kuokoa maisha ya wananchi ambao wamekuwa wakipoteza maisha kila mwaka kutokana na kupigwa na radi na kwamba tukio hilo limeleta hofu kijijini hapo.
 
Akizungumza baada ya kuongoza mazishi hayo kwa niaba ya Serikali , Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Bi.Ruth Msafiri amewataka wakazi wa kijiji hicho kutohusisha tukio hilo na imani za kishirikina na kwamba serikali itaangalia uwezekano wa kusaidiana na wananchi kuweka kinga ya kitaalam katika Taasisi za Umma zenye mikusanyiko kama shule na Zahanati.
 
Katika tukio hilo wanafunzi wanne walikufa baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani na wengine tisa kujeruhiwa katika shule ya msingi Nyaruyoba.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni