Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe,
amedai kuwa Rais Dkt John Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Nay wa
Mitego.
Dkt Mwakyembe aaedai kuwa Rais amemuambia amuelezee Nay auboreshe zaidi wimbo huo kwakuwa umegusa masuala muhimu.
“Yaani asiondoe kitu chochote, ila aongeze kwasababu unaelezea
changamoto zilizopo kwenye jamii halafu wanaitikia watu ‘wapoo’” amesema
Dkt Mwakyembe kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma leo.
“Rais amesema [Nay] amesahau vitu vingine vingi, wakwepaji kodi,
aongeze mambo kama hayo, wabwia unga na mihadarati wapo, wafanyabiashara
wa madawa ya kulevya wapo, watanzania wanaopenda tangu asubuhi hadi
jioni wao ni kwenye vijiwe tu hakuna kufanya kazi wavivu waitikie tena
wapoo.
Kwahiyo anasema itatusaidia sana maana ni muziki mzuri na BASATA
walikuwa wameshafanya mpaka uamuzi usipigwe kokote pale, wao siwalaumu
walitekeleza wajibu wao, ila leo tu nimetoka kuwaomba kipindi ambacho
mimi naongoza hii wizara naomba wafanye consultation zaidi kabla ya
kuchukua hatua ili katibu mkuu ajue, naibu waziri ajue tunaweza
kubadilishana mawazo sababu haya mambo yanahusu haki za msingi ambazo
zipo kwenye katiba ya jamhuri ya muungano,” amesisitiza Dkt Mwakyembe.
“Kwahiyo nimechukua hatua kama waziri mwenye dhamana kuwaagiza polisi
wamwachie yule kijana, hebu waache kumhoji huyu kijana, badala ya
kujitetea mimi ningemshauri hata aje Dodoma naweza kumuona kesho,
nimwelekeze vizuri hata namna ya kuongeza wimbo utakuwa mzuri kweli
kweli. Na mimi mwenyewe nimeisikiliza hii beat nakubaliana na mheshimiwa
rais, rais najua anapenda muziki, lakini hata mimi mwenyewe napenda
muziki kwakweli ile beat ni kali.”
Nay alikuwa tayari akichukuliwa maelezo na polisi jijini Dar es
Salaam. Kwa uamuzi wa Rais Magufuli hiyo ina maana kuwa hana tena shtaka
lolote la kujibu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni