Michezo hiyo ni kati ya Young Africans ya Tanzania na Zanaco ya
Zambia utakaochezwa Jumapili kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika pia
Azam FC ya Tanzania na Mbabane Swalows ya Swaziland kuwania Kombe la
Shirikisho barani Afrika.
Kwa upande wa Young Africans dhidi ya Zanaco, mchezo huo utafanyika
Jumamosi Machi 11, mwaka huu. Waamuzi kutoka Djibouti ndio
watakaochezesha mechi hiyo.
Waamuzi hao ni Djamal Aden Abdi ambaye atapuliza kipenga wakati
wasaidizi wake ni Hassan Yacin na Farhan Salime ilihali mwamuzi wa akiba
atakuwa Souleiman Djamal. Kamisha katika mchezo huo Na. 61 atakuwa
Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.
Kiingilio katika mchezo huo kwa mujibu wa Mratibu wa Mechi za
Kimataifa wa Young Africans, Mike Mike ni Sh 20,000 kwa VIP ‘A’, Sh
10,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ na Mzunguko (Viti vya Rangi ya chungwa, kijani
na bluu) ni Sh 3,000.
Azam wao watacheza Jumapili Machi 12, mwaka huu na Mbabane Swallows
ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Waamuzi watakochezesha mchezo huo wanatoka Benin ambao ni Mwamuzi wa
kati, Addissa Abdul Ligali na wasaidizi ni Medegnonwa Romains Agbodjogbe
na Babadjide Bienvenu Dina huku Mwamuzi wa akiba akiwa Moumouni Kiagou
na kamisha wa mchezo atakuwa Mohamed Omar Yusud wa Kenya.
Kiingilio katika mchezo huo kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC,
Saad Kawemba ni Sh 10,000 kwa VIP, Jukwa Kuu itakuwa ni Sh 5,000 na
Mzunguko itakuwa ni Sh 3,000.
Wakati huohuo, tiketi za waamuzi wa Tanzania walioteuliwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuchezesha mechi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika kati ya timu za AS Porto Louis 2000 ya Mauritius na El
Hilal ya Sudan wikiendi ijayo, wamepata tiketi zao za kusafiri.
Katika mchezo huo ambao utafanyika ama Machi 17, 18 au 19 Mwamuzi wa
kati atakuwa Israel Mujuni Nkongo wakati wasaidizi wake watakuwa ni
Samuel Hudson Mpenzu na Josephat Deu Bulali huku Mwamuzi wa akiba akiwa
ni Hery Sasii. Kamisha katika mchezo huo Na. 78 atakuwa Jerome Kelvyn
Damon kutoka Afrika Kusini.
Source: TFF
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni