Baada ya staa wa gospel Willy Paul Msafi kutoka nchini Kenya
anayetamba na ngoma I Do aliyomshirikisha mrembo kutoka Jamaica, Alaine
kuzulu ofisi za WCB, sasa imekuwa ni zamu ya staa mwingine wa Kenya
anayetokea mji wa zama wa pwani ya Kenya Mombasa kwa jina Chikuzee.
Chikuzee aka Zee la Mavuvuzela ni maarufu sana haswa ikizingatiwa
style yake ya muziki anayotumia kuwa ya aina yake pamoja na sauti na
mihemko inayodurusu kukamilisha burudani kamili kwenye fani ya muziki.
Mashabiki wake walifurahia punde tu Chikuzee alipokonyezea picha
alizopiga kwenye ofisi za WCB huku nyingine akiwa na CEO wa kampuni hiyo
ya muziki na staa wa kibao Marry you Diamond Platnumz.
Haijabainika wazi ni kwa madhumuni gani Chikuzee kuitembelea WCB,
lakini tetesi zipo hewani kuwa kuna kitu kiko jikoni baina ya mkali huyo
wa ngoma Si Vibaya na Raymond wa WCB. Huku wengine wakihoji kuwa huenda
alifika pale ili kutia sahihi mkataba wa kuwezesha ngoma zake kuwekwa
kwenye wavuti/tovoti ya kununua mziki ya wasafi.com.
Hata hivyo Diamond kuna kipindi alihojiwa kwenye kipindi cha Mambo
Mseto kupitia redio Citizen ya nchini Kenya na alishawahi kukiri kuwa
kati ya wasanii wa nchini Kenya anaowakubali na kuwaelewa zaidi na
hangesita kufanya kazi nao nafasi ingetokea basi Chikuzee ni mmoja wao.
Hivyo si ajabu leo hii kuona kazi ya Diamond na Chikuzee. Diamond
anazidi kuzivutia, kuzigusa na kuziongoa nyoyo za mashabiki wake haswa
wa kanda ya pwani ya Kenya kwa kuonyesha kuwa anawakubali na yuko tayari
kufanya kazi na wanamuziki wa ukanda huo pia bila kujali ukubwa alionao
kwa sasa kimuziki duniani.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni