TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumanne, 4 Oktoba 2016

PANASONIC YATAENGENEZA BETRI INAYOJIPINDA

Hakuna maoni
Betri ya Panasonic inayoweza kujipinda
Image captionBetri ya Panasonic inayoweza kujipinda
Vifaa vinavyojipinda katika soko huenda vikawa vingi kufuatia hatua ya kampuni ya Panasonic kuvumbua betri ya lithium inayoweza kujipinda katika maonyesho ya kiteknolojia nchini Japan.
Betri hiyo inaweza kutumika katika saa,bangili na nguo.Ni ndogo ,ikimaanisha haiwezi kutumika katika simu aina ya smartphone katika awamu hiyo.
Wataalam wanasema kuwa ni uvumbuzi mzuri ,ijapokuwa Panasonic sio kampuni ya kwanza kutengeza betri hizo.
Ben Wood ambaye ni mchanganuzi wa kampuni moja ya utafiti CCS ameaimbia BBC:Watengenezaji wengine kama vile LG na Samsung pia wameanzisha juhudi za kutengeza vifaa vinavyoweza kujipinda ,kama vile betri na vioo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni