TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumatatu, 3 Oktoba 2016

MZOZO WA SYRIA:MAREAKANI YASITISHA MAZUNGUMZO NA URUSI

Hakuna maoni

Madhara ya vita SyriaImage copyrightREUTERS
Image captionMadhara ya vita Syria

Marekani imetangaza kusimamisha mazungumzo na Urusi kuhusu Syria.
Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani imesema Moscow haijafuata masharti ya makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita ya kusitisha mapigano.
Imesema pia Urusi imeshindwa kuhakikishia serikali ya Syria kubaki katika makubaliano, na kuzilaumu nchi zote kuongeza mashambulizi dhidi ya raia kwa kulenga hospitali na misaada ya kibinadamu inayotolewa.
Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema imesikitishwa na uamuzi huo.
Msemaji wa wizara hiyo ameilaumu Marekani kwa kujaribu kuhamishia lawama kwa Urusi baada ya kushindwa kukidhi masharti ya makubaliano hayo yenyewe.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni