TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumatano, 5 Oktoba 2016

MAREKANI YAJIANDAA NA KIMBUNGA

Hakuna maoni
Baadhi wa wananchi wakikimbia kimbunga MatthewImage copyrightYAMIL LAGE
Image captionBaadhi wa wananchi wakikimbia kimbunga Matthew
Uhamishaji mkubwa wa watu unafanyika katika majimbo ya Florida na Carolina ya kusini nchini Marekani wakati kimbunga Matthew kikitarajiwa kuwasili nchini humo leo Alhamisi.
Kumekuwa na msongamano mkubwa barabarani katika mji wa Charleston, Carolina ya kusini ambako Gavana wa jimbo hilo ameagiza kuhamishwa kwa lazima robo ya milioni ya watu.
Rais wa Narekani Barack Obama amesema kimbunga hicho kinaweza kuwa hatari na kuwataka wakaazi wa eneo hilo kusikiliza ushauri unaotolewa na mamlaka.
Shule zimefungwa na wagonjwa wametolewa katika baadhi ya hospitali.
Kimbunga kikubwa cha mwisho kutokea na kukumba jimbo la Florida kilikuwa ni Katrina miaka 10 iliyopita.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni