Kijana mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa jimbo la kaskazin magharibi mwa Nigeria la Bauchi anasema kuwa macho yake yalitolewa na watu waliotaka kuyatumia kwa ajili ya sababu za ushirikina.
Viungo vya mwili wa binadamu ambavyo hutumiwa katika imani za uchawi ama kwa ajili ya mazingaombwe hutolea kutoka kwa watoto nchini Nigeria, na mara nyingi watu wazima huwa hawaathiriwi.
Hussain Emmanuel, ambaye kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya mji wa Bauchi, anasema shabulio lililomuacha bila uwezo wa kuona tena, lilitokea wiki mbili zilizopita katika kijiji kilichoko eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi la Tafawa Balewa.
Anasema alirubuniwa na watu wawili katika kijij cha Marti kilichopo karibu na mto waliomshawishi aende kuogelea .
Bw Emmanuel, ambaye hufanya kazi yake ya kibinafsi kama fundi wa magari, anasema alikuwa pamoja na watu hao wawili kwasababu mmoja wao alimuahidi kumpa kazi kusini mwa Nigeria.
Lakini walipokwenda mtoni walimshabulia, wakataka kumnyongana na mnyororona shingoni na baadae wakaamua kumgonga kiasi cha kupoteza fahamu.
Alipoamka, hakuweza kuona , ndipo alipopiga mayowe hadi alipookolewa na wapita njia ambao walibaini kuwa macho yake mawili yalikuwa yameondolea.
Polisi wanasema wanachunguza kisa hicho, na hawakutoa kauli yoyote kuhusiana na sababu ya washukiwa hao kutekeleza kitendo hicho.
Washukiwa wote wawili bado hawajakamatwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni