TAARIFA HUKUJUZA MENGI YA ULIMWENGUNI

Jumatano, 10 Agosti 2016

WATOTO 11 WAMEFARIKI KATIKA MOTO ULIOTOKEA HOSPITALI

Hakuna maoni


Takriban watoto 11waliozaliwa kabla ya muda wamekufa katika mkasa wa moto uliotokea katika hospitali katika mji mkuu wa iraq Baghdad, wamesema maafisa.

Ilichukua muda wa saa tatu kuzima moto huo , uliozuka usiku wa Jumanne ndani ya kitengo cha kujifunguliwa katika hospitali ya Yarmouk Hospital, katika mji wa magharibi.

Watoto wengine saba na wanawake 29 ilibidi wahamishiwe katika hospitali nyingine zilizopo karibu.
Kumi na tisa wanaaminiwa kutibiwa majeraha ya moto na hewa ya moshi waliouvuta.

Wizara ya afya inasema huenda moto huo ulisababishwa na na kasoro za umeme.

Moto unaosababishwa na umeme ni jambo la lawaida nchini Iraq kutokana na ukarabati mbovu na nyaya za umeme kuwekwa kiholela pamoja na ukosefu wa njia za kukwepa yanapotokea majanga ya moto.

Ndugu wa marehemu wenye hasira wamekusanyika nje ya hospitali Jumatano asubuhi. Wengi wameilaumu serikali kwa moto huo.

Hussein Omar, mwenye umri wa miaka, ameliambia shrika la habari la Associated Press kwamba anahofu kwamba amewapoteza watoto wake mapacha waliozaliwa wiki iliyopita.

Maafisa wa Hospitali walikua wamemwambia awaangalie kwenye hospitali nyingine mjini Baghdad, alisema.

Lakini hakuweza kuwapata na baadae aliambiwa aende kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
"nimepata vipande vipande vya mwili," Alisema Bw Omar. "nataka nirudishiwe mtoto wangu mchanga wa kiume na mtoto wangu mchanga wa kike. Serikali lazima iwarudishe kwangu."

Serikali ya Baghdad imelaumiwa kwa mkasa wa moto
Eshrak Ahmed Jaasar, mwenye umri wa miaka 41, hakuweza kumpata mpwa wake wa siku nne.
"nilikuja mapema leo asubuhi kumuona mpwa wangu na mama yake, lakini waliniambia kuhusu moto ," aliliambia shirika la AP. "mpwa wangu bado hajapatikana na mama yake amehamishiwa kwenye wodi ya hospitali nyingine."

Bi Jaasar aliongeza kuwa : "Tunawalipa maelfu ya wafanyakazi wa hospitali wa Iraq pesa ili waturuhusu tuwapatie wapendwa wetu chakula cha msingi na maziwa ambayo hawawezi kutoa."
"ni serikali fisadi ambayo haijali raia wake na ngoja hili litokee ."

Picha zinazodaiwa kuchukuliwa ndani ya hospitali ya Yarmouk zinaonyesha mende wakitamba kati kati ya sakafu zilizobomoka, uchafu uliojaa kupita kiasi kwenye mapipa ya taka, vyoo vichafu, na wagonjwa waliolala chini, shirika la habari la Reuters limeripoti.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni