Shibuda aibukia mkutano wa Rais Magufuli Mwanza.....Awapa Neno UKAWA
Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda jana alijitokeza katika mkutano wa Rais Dkt. John Magufuli katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo anatatua kero za wananchi.
Akihutubia
maelfu ya wakazi wa Mwanza na maeneo jirani waliojitokeza kumsikiliza
Rais Dkt. Magufuli , Shibuda alivitaka vyama vingine vya siasa nchini
kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa kazi anayoifanya ni kwa ajili ya
watanzania wote.
"Mheshimiwa
Rais Magufuli endelea kuwahudumia watanzania na nikuambie sijawahi
kuona mchongoma unang’olewa kwa upepo au sijawahi kuona utelezi wa
mlenda unamwangusha mtu mzima" - Alisema Shibuda.
Shibuda
alisema vyama vya UKAWA vinapaswa kutambua kwamba Rais Dkt. Magufuli ni
mtu mzuri ndiyo maana aliwasaidia kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Meya
Jijini Dar es Salaam hivyo watambue mchango wake kwa taifa .
Aidha Shibuda alimuomba Rais Magufuli kwamba akipata muda aende akamweleze vizuri matatizo yanayowakabili wakulima nchini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni