Majenerali
na wakuu wa majeshi ya nchi kavu kutoka nchi za bara la Afrika
walikutana Arusha kujadili changamoto za kiusalama katika nchi za
Afrika wameshudia mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa na jeshi la nchi kavu
la Tanzania yaliyofanyika katika eneo la mazoezi ya kijeshi wilayani
Monduli.
Miongoni mwa makamanda walioshuhudia mazoezi hayo ni Mnadhimu Mkuu
wa Jeshi la Marekani Jenerali Mark Milley na makamanda wengine ambao
kwa muda wote walionyesha kushangazwa na uwezo mkubwa wa matumizi ya
dhana za kisasa walionao askari wa Tanzania.
Wakizungumzia baada ya mazoezi hayo baadhi ya makamanda wa Jeshi la
Tanzania waliwaeleza majenerali hao kuwa mafanikio na uwezo wa Jeshi
la Tanzania ambalo limekuwa likisaidia nchi mbalimbali za Afrika ni
nidhamu na umakini wa namna ya kuwapata vijana wenye sifa ya kuwa
wanajeshi.
Majenerali na Makamanda wakuu wa majeshi ya nchi kavu kutoka nchi
za Afrika wanatarajiwa kutoa mapendekezo yao ya nanma ya kudumisha
usalama katika nchi za Afrika hapo kesho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni