Jumla ya Ng’ombe 1,294 wamekamatwa
ndani ya msitu wa taifa wa Buhindi,uliopo katika Halmashauri ya wilaya
ya Buchosa Mkoani Mwanza,huku Wafugaji kumi na saba wanaomiliki Mifugo
hiyo wakitozwa faini ya zaidi ya shilingi Milioni 200 katika zoezi la
kuondoa Mifugo iliyomo ndani ya msitu huo.
Zoezi hilo la kuondoa Mifugo hiyo ndani ya Shamba la Misitu Buhindi
limefanyika Jumapili iliyopita Machi 20,huku baadhi ya Wafugaji
wakieleza kutoridhishwa na namna zoezi hilo lilivyotekelezwa kikiwemo
kiwango kikubwa cha faini.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa,ambaye pia ni
Diwani wa Kata ya Nyanzenda Bw.Idama Kibanzi amemlalamikia Meneja wa
Msitu wa Buhindi Mohammed Hamis kwa kushindwa kutumia busara wakati wa
ukamataji wa Mifugo hiyo na kusababisha mgogoro kati ya wafugaji na
uongozi wa msitu huo.
Kaimu Katibu tawala wa wilaya ya Sengerema Aron Loshie Laizer
amefika katika msitu huo wa Taifa wa buhindi ili kujionea uharibifu
unaodaiwa kufanywa na Mifugo hiyo.
Msitu wa Buhindi uliandikishwa rasmi kisheria kuwa msitu wa hifadhi
wa taifa mwaka 1995,katika tangazo la Serikali namba 346 na una jumla
ya eneo la hekta 33,880 ambapo wanajamii wapatao 600 hujipatia ajira
kila mwaka kwenye Viwanda vya kuchakata Magogo na kupakia mbao huku watu
200 wakifanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali.
sheria hapo inabidi ifuatilie
JibuFuta